搜索
热搜: music
门户 Culture Language view content

Kiarabu

2015-6-22 23:21| view publisher: amanda| views: 4358| wiki(57883.com) 0 : 0

description: Lugha ya Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani, kwa sababu ya kutumika kwake kama lugha ya kidini kwa mamilioni ya Waslamu duniani, na kwa kutumika kwake na zaidi ya nchi ishirini na mbili ...
Lugha ya Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani, kwa sababu ya kutumika kwake kama lugha ya kidini kwa mamilioni ya Waslamu duniani, na kwa kutumika kwake na zaidi ya nchi ishirini na mbili zilizokuwemo ndani ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, mbali na kuwa ni lugha kale iliyokuwa na athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofauti tofauti duniani.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Lugha hii ambayo leo imekubaliwa kama ni mojawapo ya lugha rasmi katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, na Mkutano wa Kilele wa Kiislamu, ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno) na ufasihi mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau. Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo na mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa ni lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafdhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isiteteleke na kubadilika na kupotea kama nyingi katika lugha za ulimwengu, leo baada ya miaka zaidi ya elfu imebakia thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoteremshwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbali mbali zinazotumika na Waarabu fulani katika sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi haya yaendelee kufahamika milele na milele.

Leo, Kiarabu kinazungumzwa na watu ya zaidi ya milioni 200 kama lugha yao ya kwanza, na ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa idadi ya wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina na Kihindi na Kihispania na Kiingereza na Kibengali. Umuhimu wa lugha hii unazidi kukuwa kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Ulaya na Asia) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).
Ramani inaonyesha nchi ambako ni lugha rasmi ya pekee (kijani) au lugha rasmi pamoja na lugha nyingine (buluu)

Asili ya lugha ya Kiarabu

Kiarabu pamoja na lugha ya Kiebrania (ya Wayahudi) na Kiaramu na Kiamhari (Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi vile vile ambazo zinatokana na asili hii kama Kiashuri na Kifinisia na Kibabili na kadhalika. Baadhi ya hizi lugha zimekufa au kuwa na wazungumzi wachache, na kwa hivyo umuhimu wake umekuwa si mkubwa kama ulivyo umuhimu wa lugha ya Kiarabu.
Aina za Kiarabu

Kuna aina tatu kubwa za lugha hii ya Kiarabu: Kiarabu Fasihi ambacho kilikuwa kikitumika zama za Ujahili kabla ya kuja Uislamu, na kuendelea kutumika baada ya kuja Uislamu katika Qurani na Sunnah za Mtume Muhammad, Kiarabu Mamboleo ambacho kinatumika katika maandishi na mazungumzo rasmi baina ya Waarabu wote kwa jumla, na Kiarabu Lahaja ambacho kinatumika na watu maalumu katika sehemu fulani za nchi au vijiji, na ni lugha ya mahali tu kama vile Kiyemeni au Kimasri au Kishami au Kimaghribi, na lugha hizi au lahaja hizi zinakuwa zinatafautiana sana baina yao katika misamiati na matumizi.
Aina na Shuwa

Nigeria
Aina na Ouddai

Niger,Chad na Africa ya Mashariki.
Kiarabu fasihi

Kiarabu ni katika lugha ya zamani sana, nayo pamoja na lugha nyenginezo za Kisemiti zilikuwa zikitumika katika nchi za Mashariki ya Kati. Kiarabu ambayo tarehe yake inarudi nyuma zaidi ya miaka 2000 ni lugha kubwa yenye misamiati mengi sana na utajiri mkubwa wa maneno na misemo. Lugha Fasihi ilianza kuwa na nguvu zaidi baada ya kuteremshwa Qurani kwa lugha hio na kuhifadhiwa Hadithi za Mtume Muhammad na kuwa ndio chanzo cha lugha zote nyinginezo za Kiarabu zilizokuweko wakati huo.

Fasihi ya Kiarabu isiyo na tabia ya kidini ilikuwa hasa Ushairi. Washairi kama Abu Nuwas, Omar Khayyam, Hafiz, ibn Qayyim al-Jawziyyah kukumbukwa hadi leo. Masimulizi kama Alfu Lela U Lela hayakuwa fasihi yenyewe hata kama yamepata maarufu katika nchi za Ulaya.

Maandishi mengine ya Kiarabu yaliyokuwa muhimu sana ni maandiko ya falsafa na sayansi. Waarabu walitafsiri maandiko ya Wagiriki wa Kale wakaendeleza ujuzi wao. Katika karne zilizopita Ulaya ilipokea sehemu kubwa ya elimu yake kutoka kwa Waarabu.

Tangu karne ya 19 na katika karne ya 20 fasihi ya Kiarabu imepata uamsho mkuu. Khalil Jibran wa Lebanon yuko kati ya washairi wanaosomwa zaidi kimataifa. Nagib Mahfuz wa Misri ni mwandishi Mwarabu wa kwanza aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1988.

About us|Jobs|Help|Disclaimer|Advertising services|Contact us|Sign in|Website map|Search|

GMT+8, 2015-9-11 20:13 , Processed in 0.181165 second(s), 16 queries .

57883.com service for you! X3.1

返回顶部